Psalms 115:3-8

3 aMungu wetu yuko mbinguni,
naye hufanya lolote limpendezalo.
4 bLakini sanamu zao ni za fedha na dhahabu,
zilizotengenezwa kwa mikono ya wanadamu.
5 cZina vinywa, lakini haziwezi kusema,
zina macho, lakini haziwezi kuona;
6zina masikio, lakini haziwezi kusikia,
zina pua, lakini haziwezi kunusa;
7zina mikono, lakini haziwezi kupapasa,
zina miguu, lakini haziwezi kutembea;
wala koo zao haziwezi kutoa sauti.
8 dWale wanaozitengeneza watafanana nazo,
vivyo hivyo wale wote wanaozitumainia.
Copyright information for SwhNEN